Gari Aina Ya Toyota Rav4 Tanzania

Rav4 maana yake nini? Toyota walitumia maneno haya kiingereza
RAV4″ –“Recreational Active Vehicle with 4-wheel-drive”, ukiunganisha herufi 4 hizo za mwanzo utapata neno RAV4.
Generation ya kwanza ya Rav 4 ambayo hutumia full time 4wheel, Kuna aina mbalimbali za toyota Rav4 zinazojulikana kama Rav4 L na Rav4 J. Rav4“J” inasimama kwa “joyful” na “L” inasimama kama “liberty.”

Aina Za Toyota Rav4

Rav4 J yenye burudani , Rav 4 hii huwa na vitu vingi ndani ya gari , hata radio inayofungwa ni tofauti, na hata huwa na full time 4wheel, na seat nzuri sana ila.
Rav L husimama kama Liberty maana yake huru, gari huwa nzuri huweza kukuta ina 2wheel drive na huweza kuamua mwenyewe kubonyeza batani ya 4wheel.
Ila kuanzia 2000 Toyota ikazindua generation mpya na mfumo wa Gx na zinginezo.

Uasisi Toyota Rav 4

Panapo 1994 kampuni ya Toyota walianzia gari aina ya Rav4 ila ilikuwa kwenye category collora A110/ kabla ya kuja na mfumo SXA110. 1997/8 Toyota ikaamua kutengeneza magari kwa mfumo tofauti kabisa ya kwamba, tutengeneze cruiser ndogo zenye mfumo mlaini ambapo utumie 4wheel muda wote ambapo mtumiaji atafurahia kuendesha bila kupata shida sehemu za mchanga, tope hata milima yaani kutumia 4wheel muda wote uliingia katika ukosoaji mkubwa kuwa gari hizi hutumia mafuta mengi kutokana na injini iliyomo nyingi ni 3s engines ,na ndio ukweli na gari zenye VIDUKU, (yani ukiweka gia utasikia Kiiiiiiiiii).
Hii utokea sana pale giabox ikiinza kuchoka na kutengeneza play ndani ya giabox.

Ulaji Wa Mafuta Wa Rav4

Toyota Rav4 Kuanzia 3rd generation ni nzuri sana na wala haina tatizo lolote ikiwa utaitunza zipo za all wheel drive (AWD) na front wheel drive FWD na ina engine ya 2AZ-Fe 2400cc vilevile 2GR-Fe 3500cc na ipo pia inayotumia diesel ingawa sio common sana.
Ina CVT gearbox ambayo ni very modern technology kuwa makini wakati wa kuchange gearbox oil usiweke hizi za kawaida utaiua haraka sana hakikisha unatumia Toyota CVT oil tu.
Mambo mengine ni ya kawaida kama fuel consumption ni nzuri kwa engine ya 2AZ but 2GR ina consumption ya juu kidogo ingawa iko very powerful.
Angalia Rav4 sokoni na kama ziko sawa chukua tu lakini matunzo ni muhimu.

Kuna tofauti kati ya show room na yard Bei ya showroom ni fixed Ila bei ya gari yoyote yard inategemea na hali yake ama ishatumiwa kiasi gani, zipo za millioni 15 hadi 25. Ukiwa na bajeti nzuri ukachukua kwa millioni 32, ukiiangalia engine, body, drive train, tyres, mgurumo wa engine, everything as good kama brand new! na odo meter 68,000km.

Magari Yenye Punguzo

Tutakutumia Moja Kwa Moja Kwenye E-Mail Yako. Hii Sio Ya Kukosa!

(Strictly No Spam)