Magari Aina Ya Toyota Harrier

Magari Aina Ya Toyota Harrier

Magari aina ya Toyota Harrier Tanzania yalianza kutolewa Mwezi disemba mwaka 1997.  Kampuni ya Toyota ilitambulisha toleo jipya la gari hilo ambalo ni Toyota Harrier kwa jina lingine lexus RX ambayo ilianza kutoka 1998 mpaka mwaka 2013 na Toyota Venza ambalo ni maarufu sana America ya kasikazini ambalo lilianza kutolewa mwaka 2020 mpaka sasa. Kuanzia 1997 mpaka mwaka 2003 matoleo ya harrier yalikua katika muonekano wa “compact SUV” na kuanzia mwaka 2013 mpaka sasa muonekano uliborenywa Zaidi na kua Mid-size SUV. Mpaka sasa Toyota Harrier ina vizazi vi nne. Toleo la kwanza lilianza kutolewa mwaka 1997 mpaka mwaka 2003. Toleo la pili mwaka 2003 mpaka mwaka 2013. Toleo la tatu lilianza kutolewa mwaka 2013 mpaka mwaka 2020. Toleo la nne lilianza kutolewa mwaka 2020 na kuendelea. Katika kila toleo kuna model zenye sifa tofauti tofauti na maboresho makubwa yamefanyika katika model za iv karibuini na kufanya gari hizi zishindane na BMW na Benz M-Class katika masoko mbalimbali ulimwenguni.

Sifa Za Toyota Harrier Sokoni

Magari Aina Ya Toyota Harrier Tanzania

Harier zina engine zenye ukubwa kati ya cc 1986 na cc 3456 na yapo matoleo yenye four wheel drive na mengine hayana Unapakua makini pindi unaamua ni aina gani ya gari unataka kununua.

Ulaji wa mafuta wa harrier Model ya kwanza na la pili ni km 11 kwa lita moja. Hii ni tofauti kabisa na matoleo ya harrier new model mwaka 2013 ambapo injini zake zina performance ya hali ya juu. Na hutumia lita moja kwenda mpaka km 21.8. Maboresho hayo katika injini yalipelekea Kampuni ya Toyota kupewa tuzo ya “fuel consumption standard 2015” ambapo ilibainika kua injini z a 2.5l hybrid huokoa asilimia 20 ya mafuta.

 Kwa upande wa speed Toyota Harrier Tanzania hukimbia hadi km 180 kwa sasaa. Upande wa nafasi Toyota harrier ina nafasi yakutosha, ina milango mitano, siti tano sehemu ya kutosha kuhifadhia mizigo, na sehemu nyingine za kuhifadhia nyaraka na vitu vidogo vidogo kwenye dashboard na kadhalika. Hizi Hapa Toyota Harrier Sokoni Dar es salaam kwa bei poa

 

Vipuri Na Usalama Wa Harrier Tanzania

Toyota Harrier New Model Tanzania

Kwa bahati nzuri vipuri vya Toyota Harrier vinapatikana katika maeneo mengi Tanzania na wataalam wa kutengeza wanapatikana lakini umakini mkubwa unahitaji katika eneo ili. Usalama na Teknolojia katika matoleo ya hivi karibuni teknolojia mbalimbali zimeongezwa kama vile frequency adaptive dumpting, pre-crush safety system na stability control zimewekwa kwa usalama wa watumiaji. Teknolojia hizi huboreshwa na kuongezwa kadri muda unavyosonga

Bei Ya Toyota Harrier Tanzania

Bei ya Toyota Harrier Tanzania hutofautiana kulingana na matoleo na model ya gari. Ukitaka model ya mwanzo kuanzia mwaka 1997, gharama ya  kuliagiza ni kuanzia milioni 19 hadi kulitoa bandarini. Harrier New Model huwa na bei kubwa Zaidi, kwa mfano matoleo ya hivi karibuni bei yake ni kuanzia milioni 60 na kuendelea. bei hutofautiana kulingana na mwaka uliotengenezwa, umbali uliotembea, tofauti kati ya wauzaji na sababu nyingine ndogondogo

Harrier New Model Ikiwa Barabarani

Toyota Harrier Ikiwa Barabarani

Bei Ya Toyota Harrier New Model imechangamka na ina teknolojia nyingi, lakini unapokua barabarani ukifikisha 120km/hr au Zaid inakuwa nyepesi sana na inatabia ya kuhama njia mnoo stability inapungua hasa pale unapokua kwenye corner. Uzur wa Toyota Harrier inavutia sana umbo lake hasa kwa wakinamama wanaipenda sana. Ukipakia mzigo mzito kwenye boot yake Exel yake ya nyuma inatabia ya Kupinda hivyo tairi hulika kwa ndani mpaka urekebishe na ufanye wheel balance. Kulinganisha na Harrier, Toyota kluger ni gari ambayo haina sura nzur sana ila ni pana ndan na ukifikisha 120-150km/hr imetulia barabarani utafikiri upo 60km/hr ina stability nzuri sana.

Toyota Harrier New Model Au Kluger?

Toyota Harrier Au Klugger

Kama unataka stability na uimara, Go for kluger  au chagua Harrier New Model kama unalenga kua na gari yenye ,muonekano mzuri gari flani ya kulia bata mjini isiyotaka usumbufu.

Zingatia : unapaswa kuwa na ziada ya angalau TZS 800,000/= Ili iweze kumudu gharama zingine zitakazo ongezeka, pia malipo ya bandarini, gharama za usafirishaji na wakala atakae kutolea gari bandarini. Itakua ndani kwenye hiyo ziada (8,000,000/=)

Pia kwa sheria mpya ya sasa, gari zote inspection inapaswa kufanyika hapa hapa nchini , hivyo watakutoza pia gharama za inspection.

Pia Soma Mada Hizi Pendwa

Magari Yenye Punguzo

Tutakutumia Moja Kwa Moja Kwenye E-Mail Yako. Hii Sio Ya Kukosa!

(Strictly No Spam)