Gari aina ya IST ni gari yenye umaarufu mkubwa na inatamba katika soko la magari nchini Tanzania hasa katika jiji letu la Dar es salaam. IST imeanza kutengezwa mwaka 2002 mpaka mwaka 2007 ikiwa ni toleo la Kwanza ambapo unaweza kutambua toleo hili kutokana na modeli code NCP 60, NCP61 na NCP65 katika Chasis code zake na kuendelea kutengenezwa tena kuanzia mwaka 2007 mpaka mwaka 2016 ambapo zilisitishwa na kuanza kutengenezwa toleo la pili ambalo utalitambua kwa kuangalia model code XP110 katika Chasis .
Toyota IST imejizolea umaarufu jiji Dar es salaam na Tanzania kwa ujumla kutokana na Matumizi yake ya mafuta kuwa mazuri hivyo kusababisha IST kufanya vizuri katika Soko la Magari ndani ya Tanzania. IST hutumia mafuta kiasi cha Lita Moja kutembea Km 10 mpaka 12 mjini kwa IST yenye ukubwa wa injini ya cc1290 na cc1490 ambazo sio 4WD na lita 1 ya mafuta kwa km 13 mpaka 17 kama tu unaendesha highway huku ulaji wa mafuta ukitegemea vitu vingi kama vile tabia za uendeshaji na ubora wa gari. Umaarufu huu umesababisha Gari hili kuwa na bei ghali katika Manunuzi yake na hata unapotaka kulinunua kwa Mtu basi bei yake huwa imechangamka hata kama muuzaji ameshalitumia miaka mitano na kuendelea.
Uzuri wa Toyota IST hasa toleo la kwanza ni bei yake ya manunuzi unapotaka kuinunua bei yake sio ya ghali sana na ndio sababu watanzania wengi wameonyesha uwezo wa kuimiliki gari hii hususani vijana. Bei ya IST toleo la kwanza zinatofautiana kutokana vitu kama mwaka wa kutengenezwa gari hilo, umbali uliotembea, rangi na ubora wa gari. Katika showroom za magari hapa Dar es salaam zinakadiriwa kuanzia Shilingi Milioni 10 mpaka 13 kwa toleo la kwanza na Milioni 20 mpaka 23 kwa toleo la pili.
Umaarufu huu umesababisha Gari hili kuwa na bei ghali katika Manunuzi yake na hata unapotaka kulinunua kwa Mtu basi bei yake huwa imechangamka hata kama muuzaji ameshalitumia miaka mitano na kuendelea
IST inahitaji huduma (Service) hasa pale umbali flani unapofikia na huduma hizo ni kama vile kubadilisha Oil ya injini, Oil ya giabox, chujio la Oil (Oil Filter), Air filter, plugs na vingine kama hivyo. Gharama ya kulihudumia gari hili ni nafuu na ambayo wamiliki wengi wanaweza kuzimudu pia gari hii hutengenezeka kirahisi pindi inapotokea hitilafu katika mfumo wa injini au umeme na ndio maana gari hizi huwezi kuzikuta nyingi zikiwa gereji kwa mafundi zimepaki.
Injini ya Toyota IST zimeonyesha uimara japokuwa ni injini ambazo mara nyingi zinapokuwa zimetembea zaidi ya kilomita laki moja na nusu huanza kusumbua kwenye injini hususani katika Timing Belt ambapo inapofikisha Km laki 1 kama ilivyo kwa gari nyingi za Toyota Timing belt inahitaji kubadilishwa kutokana na kuchoka. Unapotaka kuuza gari hii basi huuzika kwa haraka kutokana na uhitaji wake kuwa mkubwa kutokana na wateja wengi kuamini kuwa ndio gari pekee inayotumia mafuta kiasi kuliko gari nyingine za muundo huo. Na ndio maana gari hizo zinapotaka kuuzwa huuzwa kwa bei karibu na bei ya kuagizwa Japan huku ikiwa imeshatumika pengine zaidi ya miaka mitano.
Soko Kubwa La Magari Tanzania
2022 © Designed by Bright Digital